Atletico Madrid jana ilifanikiwa kuiondoa AC Milan kwenye michuano ya klabu bingwa ya ulaya baada ya kuifunga 4-1 katika mchezo wa pili wa hatua ya 16 bora.
Wednesday, March 12, 2014
Hivi ndivyo akina Diego Costa walivyowanyanyasa akina Balotelli
Atletico Madrid jana ilifanikiwa kuiondoa AC Milan kwenye michuano ya klabu bingwa ya ulaya baada ya kuifunga 4-1 katika mchezo wa pili wa hatua ya 16 bora.
Kama ulimis mechi, angalia mabao ya mchezo wa Bayern vs Arsenal
Sunday, January 5, 2014
SWANSEA CITY YAIFUNGASHIA VIRAGO MAN UNITED NYUMBANI OLD TRAFORD
---------------------------------------------------------------------------------------------
![]() |
| Wayne Routledge: Broke the deadlock at Old Trafford |
Mancester united leo wamepoke kichapo cha magoli 2-1 wakiwa nyumbani old trafford kwenye michuano ya FA .Wayne Routledge's alitangulia kuifungia Swansea City goli la kuongoza dakika ya 12 lakini Javier Hernandez(Chicharito) aliisawazishia united goli hilo dakika ya 16 mechi ilibadilika pale beki wa man U Fabio alipooneshwa kadi nyekundu na Swansea city kuweza kuutawala mchezo na kupata goli la ushindi lililofungwa na mshambuliaji Wilfried Bony dakika ya 90 na kuiwezesha Swansea City kuitupa nje ya michuano ya FA.
CHEALSEA YAIFUNGA DEBY COUNTRY 2-0 RAUNDI YA NNE FA CUP
---------------------------------------------------------------------------------------------

Oscer na Willian wakishangilia kwa pamoja baada ya goli la pili kufungwa.Chelsea waliweza kuifunga Deby Countr magoli 2-0 katika michuano ya FA Cup yaliyofungwa na Obi Mikel dakika ya 66 na Oscer aliyefunga dakika ya 71.Kwa matokeo haya Chealsea sasa watakutana na Stoke City kwenye raund ya nne ya michuano hii ya FA.
HATIMAYE ROBERT LEWANDOSKI AJIUNGA NA BAYERN MUNICH KWA MKATABA WA MIAKA MITANO
-------------------------------------------------------------------------------------------------
Mshambuliaji wa Borussia Dortmund Robert Lewandowski atajiunga na klabu ya Bayern Munich kwa uhamisho huru mwishoni wa mwa msimu huu, mabingwa wa Ujerumani wametangaza.
Mshambuliaji huyo wa Poland, ambaye aliisadia Dortmund kushinda makombe mawili mfululizo ya Bundesliga 2011 na 2012, amesaini mkataba wa miaka mitano.
Mshambuliaji huyo wa Poland, ambaye aliisadia Dortmund kushinda makombe mawili mfululizo ya Bundesliga 2011 na 2012, amesaini mkataba wa miaka mitano.
Lewandowski alitangaza nia yake ya kuondoka Westfalenstadion pindi mkataba wake utakapomalizika mwishoni mwa msimu huu, na akawa anahusishwa na kujiunga na wapinzani wao Bayern.
Lewandoski, 25, alijaribu kulazimisha kuuzwa kipindi cha kiangazi kilichopita lakini Dortmund waligoma kumuuza na kusisitiza lazima amalize mkataba wake.
Mwenyekiti wa Bayern Karl-Heinz Rummenigge alitangaza dili la Lewandoski, akisema: "Tuna furaha uhamisho huu umekamilika kwa mafanikio.
"Robert Lewandowski ni mmoja ya washambuliaji bora ulimwenguni, atakiongezea ubora kikosi chetu cha FC Bayern."
Wednesday, December 4, 2013
YANGA YATOA RIPOTI YA MAPATO NA MATUMIZI
--------------------------------------------------------------------------------------------------
Uongozi wa klabu ya Young Africans leo umetoa ripoti ya mapato na
matumizi kwa kipindi cha miezi sita tangu Januari 14, 2013 mpaka
Julai 14, 2013 ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa kutoa mahesabu
hayo kwa wapenzi, washabiki, na wanachama na jamii kwa ujumla.
Wachezaji wake watano wapo katika kinyang'anyiro hicho:
Barcelona na Real Madrid wamepigwa faini ya zaidi ya£2.5million kila timu baada ya kuvunja sheria ya kusaini mkataba wa muda mrefu wa haki za matangazo ya TV.
Mikataba hiyo baina ya vilabu hivyo na kampuni ya Mediapro imevunja sheria ya nchi hiyo kupitia mamlaka ya ushindani wa kibiashara - inayokataza kuwepo kwa mkataba wa zaidi ya miaka mitatu baina ya vilabu na kampuni ya matangazo ya TV.
Comisión Nacional de la Competencia imefikia uamuzi kwamba vilabu hivyo viwili, pamoja na Sevilla na Racing Santander, vilivunja sheria iliyotungwa mwaka 2010 inayozuia mikataba ya matangazo ya TV kuzidi miaka mitatu.
Real Madrid imepigwa faini ya £3.2m na Barcelona £2.9m wakati Mediapro watalipa faini ya £5.3m. Sevilla imepigwa faini ya £745,000 na Racing Santander ambao kwa sasa wapo ligi daraja la 3 wakiwa na ukata mkubwa wa uchumi watalazimika kulipa £24,800.
Mediapro inawalipa Madrid na Barça kiasi cha £115m kwa mwaka kwa manunuzi ya haki ya mechi zao za nyumbani lakini vilabu vyote viwili vimeambiwa na mamlaka za Spain kwamba ni lazima viache kufanya dili zao binafsi za matangazo ya TV na kujiunga na vilabu vingine katika dili hizo kuanzia mwaka 2016.
Endapo Madrid na Barcelona watajiunga na vilabu vingine katika dili za matangazo ya TV basi mapato yao yatapungua.
Uongozi wa klabu ya Young Africans leo umetoa ripoti ya mapato na
matumizi kwa kipindi cha miezi sita tangu Januari 14, 2013 mpaka
Julai 14, 2013 ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa kutoa mahesabu
hayo kwa wapenzi, washabiki, na wanachama na jamii kwa ujumla.
Baadhi ya gharama kubwa kwa klabu ni pamoja na usajili wachezaji
na mishahara.Akiongea na waandishi wa habari juu ya mahesabu
hayo katibu mkuu wa Young Africans Lawrence Mwalusako
amesema mapato makubwa ya klabu yanatokana na viingilio
vya mechi na ufadhili.
- Juhudi mbalilmbali zinafanyika kuongeza kipato cha klabu kama
- kuingia mikataba ya ufadhili, kutumia haki miliki za klabu.
- Uongozi unajitahid kuweza kudhibiti matumizi ya klabu kama njia
- moja ya kuhakikisha klabu inajitegemea.
- Klabu bado inaendelea kutegemea ufadhili wa TBL ambao kwa
- sasa inapata wastani wa mIL 30.25 kila mwezi, Madhumuni ya
- ufadhili huu ni kuwezesha klabu kulipia mishahara ambayo
- wastani inzaidi mil 60 kwa mwezi. Tayari klabu imeshaomba
- mazungumzo na mfadhili kuboresha mkataba huo.
- Katika kipindi cha Januari 2013 hadi Julai 2013 klabu
- iliweza kupata mil 110 kama zwadi mbalii mbali za ushindi
- ikiwemo mil 15 kutoka vodacom kwa kuwa timu yenye nidhamu.
- Bado kuna mali za klabu hazija thaminiwa zikiwemo majengo
BALLON D'OR: KOCHA WA UJERUMANI AGOMA KUPIGA KURA ZA KUMCHAGUA MWANASOKA BORA WA DUNIA
katika mchakato wa kumchagua mwanasoka bora wa dunia
mwaka huu, shirikisho la soka la Ujerumani limethibitisha.
Wachezaji wake watano wapo katika kinyang'anyiro hicho:
Mastaa wa Bayern Munich Manuel Neuer, Philipp Lahm,
Bastian Schweinsteiger na Thomas Muller, na kiungo
wa Arsenal Mesut Ozil.
Lakini kwa sababu kura zote binafsi huwekwa hadharani
Lakini kwa sababu kura zote binafsi huwekwa hadharani
baada ya sherehe za tuzo, boss wa Mannschaft ameamua
kuepeukana na kusababisha hali ya kuonekana ana
upendeleo kwa mchezaji fulani kwa kupiga kura
hiyo ya Ballon d'Or.
"Ameshindwa kupiga kura kutokana sababu zilizo
"Ameshindwa kupiga kura kutokana sababu zilizo
nje ya uwezo wake na hivyo ameonelewa
kuepukana na zoezi hilo," msemaji wa DFB
Jens Gritter aliiambia Sport Bild.
JOPO LA MAKOCHA WAZALENDO KUPANGA MIKAKATI YA TANZANIA KUSHIRIKI AFCON 2015
JOPO LA MAKOCHA WAZALENDO KUPANGA MIKAKATI YA
TANZANIA KUSHIRIKI AFCON 2015
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi
akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja wa Bia ya Kilimnjaro,
George Kavishe na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Kidau Alfred.
Mdau wa Soka Shaffih Dauda (wa pili kulia) akiteta na makocha,
Charles Boniface Mkwasa (kulia) na Kenny Mwaisabula ambao
wamechaguliwa kuudhuria kikao maalumu kitakachofanyika
mjini Zanzibar kuanzia Desemba 6 cha kupanga mikakati
ya namna ya kuiwezesha Tanzania kushiriki Fainali za
Mataifa ya Afrika (AFCON 2015)
DAR ES SALAAM, Tanzania
RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi,
ametangaza majina 17 kati ya 20 ya Jopo la Makocha
Wazalendo watakaokutana kupanga mkakati
wa namna ya kuiwezesha
Tanzania kushiriki Fainali za Mataifa Afrika (AFCON 2015)
zitakazofanyika nchini Morocco.
Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam,
Malinzi alisema kuwa, makocha hao watakuwa na kikao
maalumu (retreat) kitakachofanyika mjini Zanzibar kwa
siku tatu kuanzia kesho Desemba 6 hadi 8, chini ya
Mwenyekiti Kanali Mstaafu Idd Kipingu.
Malinzi aliwataja makocha wanaounda jopo hilo ambalo
Katibu wake ni Pelegrinius Rutahyuga, kuwa ni
Dk. Mshindo Msolla, Peter Mhina, Ayoub Nyenzi,
Abdallah Kibadeni, Kidao Wilfred na Salum Madadi.
Makocha wengine waliotajwa na Malinzi kuwao katika jopo
hilo ni pamoja na Juma Mwambusi, Kennedy Mwaisabula
‘Mzazi’, Boniface Mkwasa, Fred Minziro, Meja Abdul Mingange,
Ally Mayay na Dan Korosso.
Malinzi alibainisha kuwa, kwa siku tatu makocha hao
watakuwa na majadiliano ya namna gani Tanzania kupitia
Taifa Stars inavyoweza kupata wachezaji wa timu za taifa
za umri tofauti watakaowezesha mchakato wa kufuzu
AFCON 2015 nchini Morocco.
“Nichukue nafasi hii kuwatakia kila la heri katika zoezi
lao, litakalojumuisha makocha watatu kutoka
Visiwani Zanzibar ambao watachaguliwa na
chama cha soka cha huko (ZFA), kisha waje na majibu
yatakayotuwezesha kufikia lengo,” alisema Malinzi.
Kwa upande wake, Meneja wa Bia ya
Kilimanjaro Premium Lager inayozalishwa na TBL,
George Kavishe, alimshukuru Malinzi kwa hatua
mbalimbali za kunyanyua soka alizoonesha tangu
alipochaguliwa na kwamba TBL inajivunia hilo.
“Kama wadhamini wa Taifa Stars, TBL inapenda kumshukuru
Malinzi kwa mkutano wake huu wa kwanza na sisi tangu alipochaguliwa,
akishirikiana na Kamati ya Utendaji na tunaamini jitihada hizi zitadumu
na kuzaa matunda,” alisema Kavishe.
Alienda mbali zaidi na kuwataka makocha waliochaguliwa
kuunda jopo hilo maalum kutambua thamani ya jukumu lao na
kuja na tiba sahihi ya matatizo yetu, huku wakitambua kwamba
wako kamatini kwa niaba ya Watanzania zaidi ya milioni 45.
Aidha, Malinzi ameunda kamati mbili maalumu (ad hoc)
kwa ajili ya kutathmini muundo wa ligi na kupendekeza
namna ya kuuboresha, na ile ya kutahmini muundo wa Bodi ya
Ligi na kupendekeza namna ya kuuboresha, ikiwemo kuunda kampuni.
Kamati ya Kutathmini Muundo wa Ligi inaongozwa na koocha wa
zamani wa Taifa Stars, Dk. Mshindo Msolla, wakati Katibu ni Ofisa
Mashindano wa TFF, Idd Mshangama. Wajumbe ni Rahim Kangezi,
Amri Said, Sunday Manara, Salim Bawazir na Lucas Kisasa.
David Nchimbi kutoka Delloitte ataongoza Kamati ya Muundo wa
Bodi ya Ligi, wakati wajumbe ni Edwin Kidifu (Mwanasheria wa SUMATRA),
Jones Paul (Mkurugenzi wa Sunderland/Symbion Academy),
Evans Aveva, John Jambele, Masoud Sanani na Pelegrinius Rutahyuga.
AFRIKA KUSINI KUTUA KWA SOUTH AFRICA AIRWAYS
Kikosi cha Afrika Kusini (Basetsana) kwa ajili ya mechi ya
mchujo ya Kombe la Dunia kwa wasichana wenye umri
chini ya miaka 20 dhidi ya Tanzania (Tanzanite) kinatua
nchini kesho (Desemba 5 mwaka huu).
Afrika Kusini itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere (JNIA) itatua saa 8 kamili mchana kwa ndege
ya South Africa Airways.
Wanaounda Basetsana ni makipa Kaylin Swart, Regirl Ngobeni
na Juliet Sethole. Mabeki ni Abongile Dlani,
Caryn van Reyneveld, Chamelle Wiltshire,
Meagan Newman, Nomonde Nomthseke,
Tiisetso Makhubela na Vuyo Mkhabela.
Viungo wapo Amanda November, Amogelang Motau,
Gabriella Salgado, Koketso Mamabolo, Nomvula Kgoale na
Thembi Kgatlane. Washambuliaji ni Mosili Makhoali,
obyn Moodaly, Sduduzo Dlamini na Shiwe Nogwanya.
Viingilio katika mechi hiyo itakayochezwa Jumamosi
(Desemba 7 mwaka huu) ni sh. 1,000 kwa viti vya rangi ya kijani,
bluu na orange, sh. 2,000 kwa VIP C, sh. 5,000
kwa VIP B wakati VIP A watalipa sh. 10,000.
TIKETI 260 KOMBE LA DUNIA BRAZIL
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limeipa Tanzania mgawo wa tiketi 260 za Fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil.
Watanzania wanaohitaji tiketi hizo wanatakiwa kutuma maombi TFF kwa maandishi wakielezea aina ya tiketi na mechi wanazotaka kushuhudia. Hakuna tiketi zitakazoombwa FIFA bila kuwepo maombi kwa maandishi.
Tiketi zilizopo kwa Tanzania ni ifuatavyo; kwa hatua ya makundi (ukiondoa mechi ya ufunguzi), raundi ya 16 bora, robo fainali na mechi ya kutafuta mshindi wa tatu ni 250.
Kwa mechi ya ufunguzi, nusu fainali mbili na fainali (mechi namba 1, 61, 52 na 64) ni tiketi kumi tu ndizo zitakazopatikana. Bei za tiketi ziko katika viwango vitatu tofauti.
Mechi ya ufunguzi tiketi zake ni dola za Marekani 495, 330 na 220. Hatua ya makundi (mechi namba 2-48) ni dola 175, 135 na 90. Hatua ya 16 bora (mechi namba 49-56) ni dola 220, 165 na 110.
Robo fainali (mechi namba 57-60) ni dola 330, 220 na 165 wakati nusu fainali (mechi namba 61 na 62) ni dola 660, 440 na 275. Mechi ya mshindi wa tatu ni dola 330, 220 na 165. Kiingilio kwa fainali kitakuwa dola 990, 660 na 440.
TFF itawasilisha maombi ya tiketi hizo FIFA kuanzia Desemba 8 mwaka huu hadi Februari 7 mwakani. Idadi ambayo itaombwa FIFA itatokana na Watanzania waliowasilisha maombi TFF kwa vile zinaweza zisipatikane tiketi zote hizo zilitengwa kwa Tanzania.
Hivyo tunasisitiza maombi ya tiketi yatakayofanyiwa kazi ni yale ambayo yamewasilishwa TFF kwa maandishi tu.
RAIS TFF AUNDA KAMATI MBILI MAALUMU
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ameunda kamati mbili maalumu (ad hoc) kwa ajili ya kutathmini muundo wa ligi na kupendekeza namna ya kuuboresha, na kutahmini muundo wa Bodi ya Ligi na kupendekeza namna ya kuuboresha ikiwemo kuunda kampuni.
Kamati ya Kutathmini Muundo wa Ligi inaongozwa na Kocha wa zamani wa Taifa Stars, Dk. Mshindo Msolla wakati Katibu ni Ofisa Mashindano wa TFF, Idd Mshangama. Wajumbe ni Rahim Kangezi, Amri Said, Sunday Manara, Salim Bawazir na Lucas Kisasa.
David Nchimbi kutoka Delloitte ndiye anayeongoza Kamati ya Muundo wa Bodi ya Ligi wakati wajumbe ni Edwin Kidifu (Mwanasheria wa SUMATRA), Jones Paul (Mkurugenzi wa Sunderland/Symbion Academy), Evans Aveva, John Jambele, Masoud Sanani na Pelegrinius Rutahyuga.
Wakati huo huo, Rais Malinzi amemteua Pelegrinius Rutahyuga kuwa Mshauri wa Rais (Ufundi). Mshauri wa Rais (Utawala) atateuliwa baadaye.
REAL MADRID NA BARCELONA WAPIGWA FAINI KWA KUVUNJA SHERIA YA MIKATABA YA HAKI ZA MATANGAZO YA TV
Barcelona na Real Madrid wamepigwa faini ya zaidi ya£2.5million kila timu baada ya kuvunja sheria ya kusaini mkataba wa muda mrefu wa haki za matangazo ya TV.
Mikataba hiyo baina ya vilabu hivyo na kampuni ya Mediapro imevunja sheria ya nchi hiyo kupitia mamlaka ya ushindani wa kibiashara - inayokataza kuwepo kwa mkataba wa zaidi ya miaka mitatu baina ya vilabu na kampuni ya matangazo ya TV.
Comisión Nacional de la Competencia imefikia uamuzi kwamba vilabu hivyo viwili, pamoja na Sevilla na Racing Santander, vilivunja sheria iliyotungwa mwaka 2010 inayozuia mikataba ya matangazo ya TV kuzidi miaka mitatu.
Real Madrid imepigwa faini ya £3.2m na Barcelona £2.9m wakati Mediapro watalipa faini ya £5.3m. Sevilla imepigwa faini ya £745,000 na Racing Santander ambao kwa sasa wapo ligi daraja la 3 wakiwa na ukata mkubwa wa uchumi watalazimika kulipa £24,800.
Mediapro inawalipa Madrid na Barça kiasi cha £115m kwa mwaka kwa manunuzi ya haki ya mechi zao za nyumbani lakini vilabu vyote viwili vimeambiwa na mamlaka za Spain kwamba ni lazima viache kufanya dili zao binafsi za matangazo ya TV na kujiunga na vilabu vingine katika dili hizo kuanzia mwaka 2016.
Endapo Madrid na Barcelona watajiunga na vilabu vingine katika dili za matangazo ya TV basi mapato yao yatapungua.
ZANZIBAR HEROES YAPIGWA NA KENYA - HATARINI KUAGA MASHINDANO YA CHELLENJI
CECAFA Challenge imezidi kushika kasi leo nchini Kenya
ambapo wenyeji Kenya wameungana na Wahabeshi wa
Ethiopia kutinga hatua ya robo fainali baada ya kuifumua
Zanzibar Heroes mabao 2-0, Uwanja wa Afrah, Nakuru.
Alikuwa ni Beki wa Azam fc, inayoshiriki ligi kuu
Alikuwa ni Beki wa Azam fc, inayoshiriki ligi kuu
Tanzania bara, Joackins Atudo aliyekuwa wa kwanza
kuandika bao la kwanza dakika ya 6 na baadaye
mshambuliaji wa AFC Leopards ya Kenya, Allan Wanga
akaandika kimiani bao la pili dakika ya 60.
Kwa matokeo ya leo, Zanzibar inabaki na alama zake
Kwa matokeo ya leo, Zanzibar inabaki na alama zake
tatu na sasa wapo mguu ndani-nje kwani watasubiri
hatima ya kwenda robo fainali katika nafasi mbili za `Best Losers`.
Kwa Harambee Stars mambo yamejipa yenyewe kwa
Kwa Harambee Stars mambo yamejipa yenyewe kwa
kutinga robo fainali kwani wametimiza alama 7 baada
ya awali kuwalaza Sudan Kusini mabao 3-1 na kutoka
suluhu na Ethiopia.
Mchezo mwingine wa kundi A uliopigwa mapema
Mchezo mwingine wa kundi A uliopigwa mapema
uliwakutanisha Sudan kusini dhidi ya Ethiopia na
kushuhudia dakika tisini zikikamilika kwa wahabeshi
kuibuka na ushindi wa mabao 2-0, uwanja wa
Afrah mjini Nakuru, Kenya.
Mabao ya Ethiopia yalifungwa na Yousuf Yassin
Mabao ya Ethiopia yalifungwa na Yousuf Yassin
aliyetokea benchi kipindi cha pili na kufunga bao
la kwanza dakika ya 54 baada ya kupokea pasi nzuri
ya Manaye Fantu kutoka upande wa kulia na
Biruk Kalbolre aliyeingia pia kipindi cha pili na
kufunga goli muhimu dakika ya 82.
Sudani Kusini sasa linakuwa Taifa la kwanza kutoa
Sudani Kusini sasa linakuwa Taifa la kwanza kutoa
mkono wa `Bai Bai` katika michuano ya mwaka huu
bila hata kupata pointi moja, kwani walifungwa
mechi zake mbili za mwanzo, 2-1 dhidi ya Zanzibar
na 3-1 kutoka kwa wenyeji Harambee stars.
Kesho shughuli inaendelea kwa timu za kundi B,
Kesho shughuli inaendelea kwa timu za kundi B,
ambapo Timu ya Taifa ya Tanzania bara,
Kilimanjaro Stars itajitupa uwanjani katika
mchezo muhimu sana dhidi ya Burundi na
Zambia watakabiliana na mabaharia wa Somalia.
KOMBE LA CHALLENGE: MCHEZO WA BURUNDI NA KILIMANJARO STARS HATARINI KUFANYIKA - AKINA TAMBWE WAFUNGIWA HOTELINI WASHINDWA KUSAFIRI
kutokana na kushindwa kulipa gharama za pango huko
nchini walipo wanaposhiriki michuano ya Cecafa Senior
Challenge Cup.
Timu hiyo ya Burundi inacheza na Kilimanjaro Stars
Timu hiyo ya Burundi inacheza na Kilimanjaro Stars
kesho Jumatano huko Nakuru lakini jioni ya leo
wamefungiwa kwenye htel ya Milele Hotel iliyopo eneo
la South ‘C’ baada ya wamiliki kukataa kuwaruhusu
kutoka kwenda Nakuru mpaka bili zitakapolipwa.
"Wakati timu nyingine zikisafiri kwenda Nakuru,
"Wakati timu nyingine zikisafiri kwenda Nakuru,
Burundi bado wamefungiwa kwenye vyumba vyao
baada ya utawala kukataa kuwaruhusu," kilisema chanzo cha habari.
Chanzo hicho cha habari kimesema kwamba
Chanzo hicho cha habari kimesema kwamba
waandaji hawajachukua hatua yoyote kutafuta
muafaka wa suala hilo. Jumapili, shirikisho la soka
la Kenya kupitia raisi wake Sam Nyamweya alisema
kwenye mahojiano na kitu kimoja cha radio kwamba
wanakabiliwa na ukata mkubwa.
AFRIKA KUSINI KUTUA ALHAMISI KUIVAA TANZANITE
Kikosi cha Afrika Kusini kwa ajili ya mechi ya mchujo ya
Kombe la Dunia kwa wasichana wenye umri chini ya miaka
20 dhidi ya Tanzania (Tanzanite) kinatua nchini
Alhamisi (Desemba 5 mwaka huu).
Afrika Kusini ambayo itafikia hoteli ya
Sapphire itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Julius Nyerere (JNIA) itatua saa 8 kamili mchana
kwa ndege ya South Africa Airways.
Mechi hiyo itachezeshwa na refa Nabikko Ssemambo
kutoka Uganda wakati mwamuzi msaidizi namba moja
ni Gebreyohanis Trhas kutoka Ethiopia. Waamuzi
wengine ambao pia wanatoka Uganda ni Nakitto
Nkumbi na Irene Namubiru.
Kamishna wa mechi hiyo ni John Muinjo kutoka Namibia.
Muinjo pia ni Mwenyekiti wa
Chama cha Mpira wa Miguu Namibia (NFA) na
mjumbe wa Kamati ya Mpira wa Miguu wa
Wanawake ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).
Viingilio katika mechi hiyo itakayochezwa
Jumamosi (Desemba 7 mwaka huu) kuanzia
saa 10 kamili jioni Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam ni sh. 1,000 kwa viti vya
rangi ya kijani, bluu na orange, sh. 2,000
kwa VIP C, sh. 5,000 kwa VIP B wakati VIP
A watalipa sh. 10,000.
Tanzanite chini ya Kocha Rogasian Kaijage inaendelea
na mazoezi kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya
Karume na ule wa Taifa kujiandaa kwa mechi hiyo.
Kambi ya Tanzanite hivi sasa imehamia
Msimbazi Hotel kutoka Ruvu mkoani Pwani.
PETER MANYIKA AVAA MEDALI YA KWANZA NCHINI OMAN
pamoja na Taifa Stars Peter Manyika amefanikiwa kuvaa medali
ya mshindi wa pili ya kombe la chama cha soka nchini Omani.
Manyika ambaye kwasasa ni kocha wa makipa wa timu ya SEEB
Manyika ambaye kwasasa ni kocha wa makipa wa timu ya SEEB
CLUB,aliiongoza timu yake kupoteza mchezo wa fainali mbele
ya timu ya SUR CLUB kwa mikwaju ya penati 3-2 baada ya timu
hizo kumaliza dakika 90 bila kufungana.
KOCHA MPYA SIMBA AANZA KAZI RASMI.
Kocha Simba, Zdravko Logarusic akiwasili kwenye mazoezi ya timu hiyo
katika Uwanja wa Kinesi jijini Dar es Salaam. Kocha huyo amesaini
mkataba wa miezi sita kuchukua nafasi ya Abdallah Kibadeni.
Zdravko Logarusic akiingia uwanjani kuanza kazi yake.
Akiwasalimia mashabiki wa Simba.
Akisalimiana na viongozi wa Simba.
Wachezaji wa Simba wakijitambulisha kwa kocha wa timu hiyo kabla
ya kuanza mazoezi.
Zoezi la kujitambulisha kwa kocha likiendelea.
Wachezaji wa Simba wakimsikiliza kocha mpya wa hiyo,
Zdravko Logarusic wakati wa mazoezi ya timu hiyo
yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Kinesi jijini Dar es Salaam.
Maelekezo ya kocha.
Kusikiliza maelekezo.
Wachezaji wakianza mazoezi.
Aliyekuwa kipa wa timu ya Yanga, Yew Berko (kushoto) akijifua na
wenzake wakati ea mazoezi ya Simba.
Aliyekuwa kipa wa timu ya Yanga, Yew Berko (kushoto) akijifua na
wenzake wakati ea mazoezi ya Simba.
Monday, December 2, 2013
Subscribe to:
Posts (Atom)















