Wednesday, December 4, 2013

YANGA YATOA RIPOTI YA MAPATO NA MATUMIZI

--------------------------------------------------------------------------------------------------
Uongozi wa klabu ya Young Africans leo umetoa ripoti ya mapato na
 matumizi kwa kipindi cha miezi sita tangu Januari 14, 2013 mpaka
 Julai 14, 2013 ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa kutoa mahesabu
 hayo kwa wapenzi, washabiki, na wanachama na jamii  kwa ujumla.
Baadhi ya gharama kubwa kwa klabu ni pamoja na usajili wachezaji
 na mishahara.Akiongea na waandishi wa habari juu ya mahesabu
 hayo katibu mkuu wa Young Africans Lawrence Mwalusako 
amesema mapato makubwa ya klabu yanatokana na viingilio
 vya mechi na ufadhili.
  • Juhudi mbalilmbali zinafanyika kuongeza kipato cha klabu kama
  •  kuingia mikataba ya ufadhili, kutumia haki miliki za klabu.
  • Uongozi unajitahid kuweza kudhibiti matumizi ya klabu kama njia
  •  moja ya kuhakikisha klabu inajitegemea.
  • Klabu bado inaendelea kutegemea ufadhili wa TBL ambao kwa
  •  sasa inapata wastani wa mIL 30.25 kila mwezi, Madhumuni ya
  •  ufadhili huu ni kuwezesha klabu kulipia mishahara ambayo
  •  wastani inzaidi mil 60 kwa mwezi. Tayari klabu imeshaomba 
  • mazungumzo na mfadhili kuboresha mkataba huo.
  • Katika kipindi cha Januari 2013 hadi Julai 2013 klabu
  •  iliweza kupata mil 110 kama zwadi mbalii mbali za ushindi 
  • ikiwemo mil 15 kutoka vodacom kwa kuwa timu yenye nidhamu.
  •  Bado kuna mali za klabu hazija thaminiwa zikiwemo majengo
 

BALLON D'OR: KOCHA WA UJERUMANI AGOMA KUPIGA KURA ZA KUMCHAGUA MWANASOKA BORA WA DUNIA

Kocha wa
timu ya taifa ya Ujerumani Joachim Low amekataa kupiga kura  
katika mchakato wa kumchagua mwanasoka bora wa dunia
 mwaka huu, shirikisho la soka la Ujerumani limethibitisha. 

Wachezaji wake watano wapo katika kinyang'anyiro hicho: 
Mastaa wa Bayern Munich Manuel Neuer, Philipp Lahm,
 Bastian Schweinsteiger na Thomas Muller, na kiungo 
wa Arsenal Mesut Ozil.

Lakini kwa sababu kura zote binafsi huwekwa hadharani 
baada ya sherehe za tuzo, boss wa Mannschaft ameamua
 kuepeukana na kusababisha hali ya kuonekana ana 
upendeleo kwa mchezaji fulani kwa kupiga kura
 hiyo ya Ballon d'Or.

"Ameshindwa kupiga kura kutokana sababu zilizo 
nje ya uwezo wake na hivyo ameonelewa 
kuepukana na zoezi hilo," msemaji wa DFB 
 Jens Gritter aliiambia Sport Bild.

JOPO LA MAKOCHA WAZALENDO KUPANGA MIKAKATI YA TANZANIA KUSHIRIKI AFCON 2015

JOPO LA MAKOCHA WAZALENDO KUPANGA MIKAKATI YA
 TANZANIA KUSHIRIKI AFCON 2015
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi
 akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa 
habari jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja wa Bia ya Kilimnjaro,
 George Kavishe na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Kidau Alfred. 
Mdau wa Soka Shaffih Dauda (wa pili kulia) akiteta na makocha,
 Charles Boniface Mkwasa (kulia) na Kenny Mwaisabula ambao 
wamechaguliwa kuudhuria kikao maalumu kitakachofanyika 
mjini Zanzibar kuanzia Desemba 6 cha kupanga mikakati
 ya namna ya kuiwezesha Tanzania kushiriki Fainali za 
Mataifa ya Afrika (AFCON 2015)

DAR ES SALAAM, Tanzania

RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi,
 ametangaza majina 17 kati ya 20 ya Jopo la Makocha 
Wazalendo watakaokutana kupanga mkakati 
wa namna ya kuiwezesha
Tanzania kushiriki Fainali za Mataifa Afrika (AFCON 2015)
 zitakazofanyika nchini Morocco.
Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam,
Malinzi alisema kuwa, makocha hao watakuwa na kikao 
maalumu (retreat) kitakachofanyika mjini Zanzibar kwa 
siku tatu kuanzia kesho Desemba 6 hadi 8, chini ya
 Mwenyekiti Kanali Mstaafu Idd Kipingu.

Malinzi aliwataja makocha wanaounda jopo hilo ambalo 
Katibu wake ni Pelegrinius Rutahyuga, kuwa ni 
Dk. Mshindo Msolla, Peter Mhina, Ayoub Nyenzi, 
Abdallah Kibadeni, Kidao Wilfred na Salum Madadi.

Makocha wengine waliotajwa na Malinzi kuwao katika jopo 
hilo ni pamoja na Juma Mwambusi, Kennedy Mwaisabula 
‘Mzazi’, Boniface Mkwasa, Fred Minziro, Meja Abdul Mingange, 
Ally Mayay na Dan Korosso.
Malinzi alibainisha kuwa, kwa siku tatu makocha hao 
watakuwa na majadiliano ya namna gani Tanzania kupitia 
Taifa Stars inavyoweza kupata wachezaji wa timu za taifa
 za umri tofauti watakaowezesha mchakato wa kufuzu
AFCON 2015 nchini Morocco.

“Nichukue nafasi hii kuwatakia kila la heri katika zoezi 
lao, litakalojumuisha makocha watatu kutoka 
Visiwani Zanzibar ambao watachaguliwa na
 chama cha soka cha huko (ZFA), kisha waje na majibu 
yatakayotuwezesha kufikia lengo,” alisema Malinzi.

Kwa upande wake, Meneja wa Bia ya 
Kilimanjaro Premium Lager inayozalishwa na TBL,
 George Kavishe, alimshukuru Malinzi kwa hatua 
mbalimbali za kunyanyua soka alizoonesha tangu 
alipochaguliwa na kwamba TBL inajivunia hilo.

“Kama wadhamini wa Taifa Stars, TBL inapenda kumshukuru 
Malinzi kwa mkutano wake huu wa kwanza na sisi tangu alipochaguliwa, 
akishirikiana na Kamati ya Utendaji na tunaamini jitihada hizi zitadumu
 na kuzaa matunda,” alisema Kavishe.

Alienda mbali zaidi na kuwataka makocha waliochaguliwa 
kuunda jopo hilo maalum kutambua thamani ya jukumu lao na 
kuja na tiba sahihi ya matatizo yetu, huku wakitambua kwamba
wako kamatini kwa niaba ya Watanzania zaidi ya milioni 45.

Aidha, Malinzi ameunda kamati mbili maalumu (ad hoc)
 kwa ajili ya kutathmini muundo wa ligi na kupendekeza 
namna ya kuuboresha, na ile ya kutahmini muundo wa Bodi ya
Ligi na kupendekeza namna ya kuuboresha, ikiwemo kuunda kampuni.

Kamati ya Kutathmini Muundo wa Ligi inaongozwa na koocha wa 
zamani wa Taifa Stars, Dk. Mshindo Msolla, wakati Katibu ni Ofisa 
Mashindano wa TFF, Idd Mshangama. Wajumbe ni Rahim Kangezi,
 Amri Said, Sunday Manara, Salim Bawazir na Lucas Kisasa.

David Nchimbi kutoka Delloitte ataongoza Kamati ya Muundo wa 
Bodi ya Ligi, wakati wajumbe ni Edwin Kidifu (Mwanasheria wa SUMATRA),
 Jones Paul (Mkurugenzi wa Sunderland/Symbion Academy), 
Evans Aveva, John Jambele, Masoud Sanani na Pelegrinius Rutahyuga.

AFRIKA KUSINI KUTUA KWA SOUTH AFRICA AIRWAYS

Kikosi cha Afrika Kusini (Basetsana) kwa ajili ya mechi ya 
mchujo ya Kombe la Dunia kwa wasichana wenye umri 
chini ya miaka 20 dhidi ya Tanzania (Tanzanite) kinatua 
nchini kesho (Desemba 5 mwaka huu).

Afrika Kusini itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
 Julius Nyerere (JNIA) itatua saa 8 kamili mchana kwa ndege 
ya South Africa Airways.

Wanaounda Basetsana ni makipa Kaylin Swart, Regirl Ngobeni 
na Juliet Sethole. Mabeki ni Abongile Dlani, 
Caryn van Reyneveld, Chamelle Wiltshire, 
Meagan Newman, Nomonde Nomthseke, 
Tiisetso Makhubela na Vuyo Mkhabela.

Viungo wapo Amanda November, Amogelang Motau, 
Gabriella Salgado, Koketso Mamabolo, Nomvula Kgoale na 
Thembi Kgatlane. Washambuliaji ni Mosili Makhoali, 
obyn Moodaly, Sduduzo Dlamini na Shiwe Nogwanya.

Viingilio katika mechi hiyo itakayochezwa Jumamosi
 (Desemba 7 mwaka huu) ni sh. 1,000 kwa viti vya rangi ya kijani,
 bluu na orange, sh. 2,000 kwa VIP C, sh. 5,000 
kwa VIP B wakati VIP A watalipa sh. 10,000.

TIKETI 260 KOMBE LA DUNIA BRAZIL

Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limeipa Tanzania mgawo wa tiketi 260 za Fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil.

Watanzania wanaohitaji tiketi hizo wanatakiwa kutuma maombi TFF kwa maandishi wakielezea aina ya tiketi na mechi wanazotaka kushuhudia. Hakuna tiketi zitakazoombwa FIFA bila kuwepo maombi kwa maandishi.

Tiketi zilizopo kwa Tanzania ni ifuatavyo; kwa hatua ya makundi (ukiondoa mechi ya ufunguzi), raundi ya 16 bora, robo fainali na mechi ya kutafuta mshindi wa tatu ni 250.

Kwa mechi ya ufunguzi, nusu fainali mbili na fainali (mechi namba 1, 61, 52 na 64) ni tiketi kumi tu ndizo zitakazopatikana. Bei za tiketi ziko katika viwango vitatu tofauti.

Mechi ya ufunguzi tiketi zake ni dola za Marekani 495, 330 na 220. Hatua ya makundi (mechi namba 2-48) ni dola 175, 135 na 90. Hatua ya 16 bora (mechi namba 49-56) ni dola 220, 165 na 110.

Robo fainali (mechi namba 57-60) ni dola 330, 220 na 165 wakati nusu fainali (mechi namba 61 na 62) ni dola 660, 440 na 275. Mechi ya mshindi wa tatu ni dola 330, 220 na 165. Kiingilio kwa fainali kitakuwa dola 990, 660 na 440.

TFF itawasilisha maombi ya tiketi hizo FIFA kuanzia Desemba 8 mwaka huu  hadi Februari 7 mwakani. Idadi ambayo itaombwa FIFA itatokana na Watanzania waliowasilisha maombi TFF kwa vile zinaweza zisipatikane tiketi zote hizo zilitengwa kwa Tanzania.

Hivyo tunasisitiza maombi ya tiketi yatakayofanyiwa kazi ni yale ambayo yamewasilishwa TFF kwa maandishi tu.

RAIS TFF AUNDA KAMATI MBILI MAALUMU

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ameunda kamati mbili maalumu (ad hoc) kwa ajili ya kutathmini muundo wa ligi na kupendekeza namna ya kuuboresha, na kutahmini muundo wa Bodi ya Ligi na kupendekeza namna ya kuuboresha ikiwemo kuunda kampuni.

Kamati ya Kutathmini Muundo wa Ligi inaongozwa na Kocha wa zamani wa Taifa Stars, Dk. Mshindo Msolla wakati Katibu ni Ofisa Mashindano wa TFF, Idd Mshangama. Wajumbe ni Rahim Kangezi, Amri Said, Sunday Manara, Salim Bawazir na Lucas Kisasa.

David Nchimbi kutoka Delloitte ndiye anayeongoza Kamati ya Muundo wa Bodi ya Ligi wakati wajumbe ni Edwin Kidifu (Mwanasheria wa SUMATRA), Jones Paul (Mkurugenzi wa Sunderland/Symbion Academy), Evans Aveva, John Jambele, Masoud Sanani na Pelegrinius Rutahyuga.

Wakati huo huo, Rais Malinzi amemteua Pelegrinius Rutahyuga kuwa Mshauri wa Rais (Ufundi). Mshauri wa Rais (Utawala) atateuliwa baadaye.

REAL MADRID NA BARCELONA WAPIGWA FAINI KWA KUVUNJA SHERIA YA MIKATABA YA HAKI ZA MATANGAZO YA TV


Barcelona na Real Madrid wamepigwa faini ya zaidi ya£2.5million kila timu baada ya kuvunja sheria ya kusaini mkataba wa muda mrefu wa haki za matangazo ya TV.

Mikataba hiyo baina ya vilabu hivyo na kampuni ya Mediapro imevunja sheria ya nchi hiyo kupitia mamlaka ya ushindani wa kibiashara - inayokataza kuwepo kwa mkataba wa zaidi ya miaka mitatu baina ya vilabu na kampuni ya matangazo ya TV.

 Comisión Nacional de la Competencia imefikia uamuzi kwamba vilabu hivyo viwili, pamoja na Sevilla na Racing Santander, vilivunja sheria iliyotungwa mwaka 2010 inayozuia mikataba ya matangazo ya TV kuzidi miaka mitatu.

Real Madrid imepigwa faini ya £3.2m na Barcelona £2.9m wakati Mediapro watalipa faini ya  £5.3m. Sevilla imepigwa faini ya  £745,000 na Racing Santander ambao kwa sasa wapo ligi daraja la 3 wakiwa na ukata mkubwa wa uchumi watalazimika kulipa £24,800.

Mediapro inawalipa Madrid na Barça kiasi cha £115m kwa mwaka kwa manunuzi ya haki ya mechi zao za nyumbani lakini vilabu vyote viwili vimeambiwa na mamlaka za Spain kwamba ni lazima viache kufanya dili zao binafsi za matangazo ya TV na kujiunga na vilabu vingine katika dili hizo kuanzia mwaka 2016.

Endapo Madrid na Barcelona watajiunga na vilabu vingine katika dili za matangazo ya TV basi mapato yao yatapungua. 


ZANZIBAR HEROES YAPIGWA NA KENYA - HATARINI KUAGA MASHINDANO YA CHELLENJI

Harambee-Stars
Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe.COM
MICHUANO ya kombe la Mataifa ya Afrika mashariki na kati,
 CECAFA Challenge imezidi kushika kasi leo nchini Kenya
 ambapo wenyeji Kenya wameungana na Wahabeshi wa
 Ethiopia kutinga hatua ya robo fainali baada ya kuifumua 
Zanzibar Heroes mabao 2-0, Uwanja wa Afrah, Nakuru.

Alikuwa ni Beki wa Azam fc, inayoshiriki ligi kuu 
Tanzania bara, Joackins Atudo aliyekuwa wa kwanza
 kuandika bao la kwanza dakika ya 6 na baadaye 
mshambuliaji wa AFC Leopards ya Kenya, Allan Wanga 
akaandika kimiani bao la pili dakika ya 60.

Kwa matokeo ya leo, Zanzibar inabaki na alama zake
 tatu na sasa wapo mguu ndani-nje kwani watasubiri
 hatima ya kwenda robo fainali katika nafasi mbili za `Best Losers`.

Kwa Harambee Stars mambo yamejipa yenyewe kwa 
kutinga robo fainali kwani wametimiza alama 7 baada 
ya awali kuwalaza Sudan Kusini mabao 3-1 na kutoka
 suluhu na Ethiopia.

Mchezo mwingine wa kundi A uliopigwa mapema 
uliwakutanisha Sudan kusini dhidi ya Ethiopia na
 kushuhudia dakika tisini zikikamilika kwa wahabeshi
 kuibuka na ushindi wa mabao 2-0, uwanja wa
 Afrah mjini Nakuru, Kenya.

Mabao ya Ethiopia yalifungwa na Yousuf Yassin 
aliyetokea benchi kipindi cha pili na kufunga bao
la kwanza dakika ya 54 baada ya kupokea pasi nzuri
ya Manaye Fantu kutoka upande wa kulia na 
Biruk Kalbolre aliyeingia pia kipindi cha pili na
 kufunga goli muhimu dakika ya 82.

Sudani Kusini sasa linakuwa Taifa la kwanza kutoa 
mkono wa `Bai Bai` katika michuano ya mwaka huu 
bila hata kupata pointi moja, kwani walifungwa 
mechi zake mbili za mwanzo, 2-1 dhidi ya Zanzibar
 na 3-1 kutoka kwa wenyeji Harambee stars.

Kesho shughuli inaendelea kwa timu za kundi B, 
ambapo Timu ya Taifa ya Tanzania bara, 
Kilimanjaro Stars itajitupa uwanjani katika 
mchezo muhimu sana dhidi ya Burundi na 
Zambia watakabiliana na mabaharia wa Somalia.

KOMBE LA CHALLENGE: MCHEZO WA BURUNDI NA KILIMANJARO STARS HATARINI KUFANYIKA - AKINA TAMBWE WAFUNGIWA HOTELINI WASHINDWA KUSAFIRI

Timu ya taifa ya Burundi imezuiliwa kwenye hotel waliyofikia 
kutokana na kushindwa kulipa gharama za pango huko
 nchini walipo wanaposhiriki michuano ya Cecafa Senior 
Challenge Cup.

Timu hiyo ya Burundi inacheza na Kilimanjaro Stars 
kesho Jumatano huko Nakuru lakini jioni ya leo 
wamefungiwa kwenye htel ya Milele Hotel iliyopo eneo
 la South ‘C’ baada ya wamiliki kukataa kuwaruhusu 
kutoka kwenda Nakuru mpaka bili zitakapolipwa.

"Wakati timu nyingine zikisafiri kwenda Nakuru, 
Burundi bado wamefungiwa kwenye vyumba vyao
 baada ya utawala kukataa kuwaruhusu," kilisema chanzo cha habari.

Chanzo hicho cha habari kimesema kwamba 
waandaji hawajachukua hatua yoyote kutafuta 
muafaka wa suala hilo. Jumapili, shirikisho la soka 
la Kenya kupitia raisi wake Sam Nyamweya alisema 
kwenye mahojiano na kitu kimoja cha radio kwamba 
wanakabiliwa na ukata mkubwa.

YAYA TOURE ATANGAZWA KUWA MCHEZAJI BORA WA AFRIKA. UNADHANI ALISTAHILI KULIKO JOHN OBI MIKEL? JADILI KWA VIGEZO.



AFRIKA KUSINI KUTUA ALHAMISI KUIVAA TANZANITE


Kikosi cha Afrika Kusini kwa ajili ya mechi ya mchujo ya
Kombe la Dunia kwa wasichana wenye umri chini ya miaka 
20 dhidi ya Tanzania (Tanzanite) kinatua nchini 
Alhamisi (Desemba 5 mwaka huu).

Afrika Kusini ambayo itafikia hoteli ya 
Sapphire itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa 
wa Julius Nyerere (JNIA) itatua saa 8 kamili mchana 
kwa ndege ya South Africa Airways.

Mechi hiyo itachezeshwa na refa Nabikko Ssemambo
 kutoka Uganda wakati mwamuzi msaidizi namba moja
 ni Gebreyohanis Trhas kutoka Ethiopia. Waamuzi 
wengine ambao pia wanatoka Uganda ni Nakitto 
Nkumbi na Irene Namubiru.

Kamishna wa mechi hiyo ni John Muinjo kutoka Namibia.
 Muinjo pia ni Mwenyekiti wa 
Chama cha Mpira wa Miguu Namibia (NFA) na 
mjumbe wa Kamati ya Mpira wa Miguu wa 
Wanawake ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).

Viingilio katika mechi hiyo itakayochezwa 
Jumamosi (Desemba 7 mwaka huu) kuanzia 
saa 10 kamili jioni Uwanja wa Taifa, 
Dar es Salaam ni sh. 1,000 kwa viti vya 
rangi ya kijani, bluu na orange, sh. 2,000 
kwa VIP C, sh. 5,000 kwa VIP B wakati VIP 
A watalipa sh. 10,000.

Tanzanite chini ya Kocha Rogasian Kaijage inaendelea 
na mazoezi kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya
 Karume na ule wa Taifa kujiandaa kwa mechi hiyo. 
Kambi ya Tanzanite hivi sasa imehamia 
Msimbazi Hotel kutoka Ruvu mkoani Pwani.

PETER MANYIKA AVAA MEDALI YA KWANZA NCHINI OMAN


Golikipa wa zamani wa vilabu vya Sigara,Yanga na Mtibwa Sugar 
pamoja na Taifa Stars Peter Manyika amefanikiwa kuvaa medali 
ya mshindi wa pili ya kombe la chama cha soka nchini Omani.

Manyika ambaye kwasasa ni kocha wa makipa wa timu ya SEEB 
CLUB,aliiongoza timu yake kupoteza mchezo wa fainali mbele 
ya timu ya SUR CLUB kwa mikwaju ya penati 3-2 baada ya timu 
hizo kumaliza dakika 90 bila kufungana.

KOCHA MPYA SIMBA AANZA KAZI RASMI.

 Kocha Simba, Zdravko Logarusic akiwasili kwenye mazoezi ya timu hiyo
  katika Uwanja wa Kinesi jijini Dar es Salaam. Kocha huyo amesaini 
mkataba wa miezi sita kuchukua nafasi ya Abdallah Kibadeni.
  Zdravko Logarusic akiingia uwanjani kuanza kazi yake.
Akiwasalimia mashabiki wa Simba.
 Akisalimiana na viongozi wa Simba.
 Wachezaji wa Simba wakijitambulisha kwa kocha wa timu hiyo kabla 
ya kuanza mazoezi.
 Zoezi la kujitambulisha kwa kocha likiendelea.
 Wachezaji wa Simba wakimsikiliza kocha mpya wa hiyo, 
Zdravko Logarusic wakati wa mazoezi ya timu hiyo 
yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Kinesi jijini Dar es Salaam.
 Maelekezo ya kocha.
 Kusikiliza maelekezo.
 Wachezaji wakianza mazoezi.
 Aliyekuwa kipa wa timu ya Yanga, Yew Berko (kushoto) akijifua na 
wenzake wakati ea mazoezi ya Simba.
 Aliyekuwa kipa wa timu ya Yanga, Yew Berko (kushoto) akijifua na 
wenzake wakati ea mazoezi ya Simba.

No comments:

Post a Comment