Monday, October 28, 2013

BREAKING NEWS:JAMAL MALINZI NDIYE RAIS MPYA WA TFF

-----------------------------------------------------------------------------------------------------

Jamal Malinz

Jamal Emil Malinzi ndiye Rais mpya wa Shirikisho la Mpira wa MiguuTanzania (TFF) baada ya kuibuka kidedea katika uchaguzi mkuu washirikisho hilo kwa kupata kura 73 kati ya kura 126 zilizopigwa, dhidi yampinzania wake Athumani Nyamlani aliyepata kura 52 kwenye
kinyang'anyiro hicho kilichohitimishwa usiku wa kuamkia leo katika jengola NSSF la Waterfront jijini Dar es salaam.Malinzi ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha soka cha mkoa wa Kageraameshinda uchaguzi huo ikiwa ni mara yake ya pili kugombea baada yakushindwa na Rais wa zamani wa TFF Leodgar Chillah tenga mwaka2008.Nafasi ya Makamu wa Rais imenyakuliwa na Wallace Kiriaaliyemshinda Ramadhani Nasib kwa kura 67 dhidi ya 52, wakati mgombeamwingine katika nafasi hiyo Imani Mahugila Madega kapata kuta 6.Katika nafasi za Ujumbe; Kanda ya 13; kiungo wa zamani wa Simba SCWilfred Kidau amepata kura 60 na kuwashinda Muhsin Said kura 50, OmarAbdulkadir kura 10 na Alex Kabuzelia kura nne. Kanda 12; Khalid MohamedAbdallah amepata kura 69 na kumshinda Davies Mosha aliyepata kura 54.Kanda ya 11 Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ amepata kura 78 na kuwashindaRiziki Majala kura tano, Twahir Njoki kura mbili, Juma Pinto kura 26 naFarid Mbaraka kura 14, Kanda ya 10 ameshinda Hussein Mwamba aliyepatakura 63, huku Charles Komba akipata nne na Stewart Nasima 58.Kanda ya tisa Othman Kambi aliyepata kura 84 yeye amewashinda FrancisBulame kura 30, wakati James Mhagama aliyepata 93 amemshinda ZafaraniDamoda aliyepata kura 11 na Kanda ya nane, Ngube Kiondo amepata kura 73amemshinda Ayoub Nyaulingo kura 52.Kanda ya Tano, Ahmed Iddi Mgoyi aliyepata kura 92 amemshinda YussufKitumbo aliyepata kura 34, wakati Kanda Omar Walii Ali amepata kura 53dhidi ya 19 za Ally Mtumwa.Eley Mbise amepata kura 51 dhidi ya 53 kura 57 za Lamanda Swai. MbashaMatutu aliyepata kura 63, amembwaga Vesastis Ligano aliyepata kura 61,wakati Vedastus Lufano aliyepata kura 51, amewashinda Jumbe OdesaMagati kura 11, Mugisha Galibona kura 24 na Samuel Nyalla kura 39 naKanda namba moja, Karilo Samson hakuwa na mpizani akapita moja kwa moja.


                        Rais mpya wa TFF Jamal Malinzi akiwa na Dream Team yake baada ya uchaguzi

No comments:

Post a Comment